Duration 8:16

Mzee Makamba Azungumza Kifo Cha Magufuli Amtumia Ujumbe Mama Samia Utabeba Mzigo wa Matatizo ya waTz

41 206 watched
0
116
Published 18 Mar 2021

Ujumbe wa Yusuph Makamba kifo cha Rais Magufuli Mhe Makamu wa Rais, nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais wetu na Mwenyekiti wetu wa Ccm Mhe John Pombe Magufuli. Msiba huu umeniumiza sana. Naleta kwako binafsi salamu za pole, kwa familia ya marehemu, kwa Watanzania wote, Viongozi wa Ccm na Wanachama wote wa Ccm. Umepata msiba mkubwa unaoumiza. Mungu akupe uvumilivu, utabeba mzigo mzito wa matatizo, usiogope. Mungu anapowatwisha watu mizigo mizito ya matatizo, huwajaaliya mabega mazito na imara ya kubeba mzigo huo mzito. Mungu atakujaaliya mabega mazito na imara ya kuubeba mzigo huu. Mungu amjaaliye pepo ya daraja marehemu John Pombe Magufuli. Innalillahi wainna ilaihi raajiuuna. Mungu ametoa na Mungu ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe. Ni Mzee Yussuf R Makamba, Katibu Mkuu Mstaafu wa Ccm, Tegeta Dsm.

Category

Show more

Comments - 36